Aug 09, 2019 12:09 UTC
  • Umoja wa Mataifa wataka kusitishwa mapigano huko Libya

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya umetoa wito wa kusitishwa mapigano kwa sababu za kibinadamu huko Tripoli mji mkuu wa Libya.

Taarifa hiyo ya Umoja wa Mataifa imezitaka pande zote zinazozozana huko Tripoli zikubali usitsihaji mapigano kwa sababu za kibinadamu kwa mnasaba wa maadhimisho ya Sikukuu ya Idul-Adhha ambayo nchini humo yataanza Jumapili tarehe 11 Agosti. Umoja wa Mataifa umesema unataraji kuwa pande zinazozozana huko Tripoli zitafikia makubaliano ya kimaandishi.   

Wanamgambo wa kundi linalojiita jeshi la kitaifa la Libya wanaoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar walianza kutekeleza mashambulizi ya anga na nchi kavu katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli Aprili 4 mwaka huu wakisaidiwa na Saudi Arabia, Imarati, Misri na Marekani kwa lengo la kuudihibiti mji mkuu huo. Hata hivyo kundi hilo limeshindwa kufikai lengo lake kutokana na kukabiliwa na vikosi vinavyoiunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya. 

Jenerali Khalifa Haftar, Kamanda wa wanamgambo kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya 
 

Libya imetumbukia katika hali ya mchafukoge na mgogoro wa kisiasa  mwaka 2011 baada ya kupinduliwa utawala wa Muammar Gaddafi dikteta wa zamani nchi hiyo kwa uingiliaji kati wa Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya na za Kiarabu. 

Tags

Maoni