Aug 31, 2019 02:42 UTC
  • Wahariji 155 wa Kiafrika wamiminika kaskazini mwa Morocco

Viongozi wa eneo la Ceuta linalodhibitiwa na Uhispania lililoka kaskasini mwa Morocco wametangaza kuwa kundi moja kubwa la wahajiri wa Kiafrika limeingia kwenye eneo hilo kinyume cha sheria.

Msemaji mmoja rasmi wa eneo hilo la kaskazini mwa Morocco ambalo liko mikononi mwa Uhispania amesema kuwa, wahajiri wote hao 155 ambao jana Ijumaa walovuuka vizuizi vyote vya mpakani na kuingia kwenye eneo hilo ni kutoka nchi zilizoko chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika na wengi wao ni raia wa Guinea Conakry. Jana wahajiri hao walitumia hali ya hewa ya ukungu na kiza kuvuka mpaka na kuingia katika eneo hilo na kuwajeruhi walinzi 12 wa mpakani waliojaribu kuwazuia wasilivamie eneo hilo.

Viongozi wa Ceuta wamesema kuwa, hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kuweza wahajiri haramu kuingia kundi zima kwenye eneo hilo.

 

Miji ya Ceuta na Melilla ina utawala wa ndani na iko chini ya serikali ya Uhispania licha ya kwamba kijiografia iko kaskazini mwa Morocco. Miji hiyo ndio mpaka pekee wa ardhini baina ya bara la Afrika na nchi za Ulaya. 

Takwimu za karibuni kabisa za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uhispania zinaonesha kuwa, wahajiri 427 wamefanikiwa kuingia katika miji hiyo miwili tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2019 hadi hivi sasa.

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Wahajiri, mwaka 2018 Uhispania ilikuwa lango kuu la kuingia wahajiri haramu barani Ulaya lakini mwaka huu wahajiri wengi wanatumia mipaka wa Ugiriki kuingia barani Ulaya.

Tags

Maoni