Sep 03, 2019 08:07 UTC
  • Agnes Callamard
    Agnes Callamard

Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa matatizo ya kiusalama ya Nigeria yametengeneza mgogoro ambao unahitajia kupewa mazingatio haraka iwezekanavyo, la sivyo utasababisha ukosefu wa usalama katika nchi nyingine za Kiafrika.

Agnes Callamard amesema kuwa Nigeria imekuwa kama chungu za migogoro ya ndani na kwamba hali inayotawala nchini humo inatia wasiwasi mkubwa.

Callamard ambaye amekuwa katika safari ya kikazi ya siku 12 nchini Nigeria amesema kuwa, polisi na jeshi la Nigeria linatumia nguvu na mabavu kupita kiasi katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika vinavyoambata kutofanyika uchunguzi wa kutosha na uwajibikaji.

Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kunyonga watu bila ya kufikishwa mahakamani, amesisitiza kuwa, Nigeria inahitajia marekebisho katika taasisi za mahakama, polisi na jeshi ili kukomesha mwenendo wa wananchi kutumia mabavu kutokana na kutopata haki na uadilifu.

Agnes Callamard

Callamard pia amekosoa alichosema ni kunyimwa maisha kwa mabavu na utumiaji wa nguvu kupita kiasi dhidi ya mikusanyiko ya wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN). Amesema hatua ya kupigwa marufuku harakati hiyo ya Kiislamu inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky ilitegemea dhana tu na kwamba hajapewa ushahidi wowote wa kuthibitisha kuwa kundi hilo lina silaha au ni hatari kwa Nigeria.   

Tags