Sep 12, 2019 04:05 UTC
  • Kongamano la 5 la Uwekezaji Afrika lafanyika Congo Brazaville

Kongamano la 5 la uwekezaji barani Afrika linamalizika leo Alhamisi huko Brazzaville, Jamhuri ya Kongo, ambapo washiriki wameangazia kwa kina ushirikiano wa uchumi anuwai na utoaji wa nafasi za ajira kwenye uchumi wa Afrika.

Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amesema, kongamano hilo limefanyika katika wakati muafaka kwani bara hilo liko katika kipindi muhimu cha kutekeleza makubaliano ya maeneo ya biashara huria ya Afrika AfCFTA, ambayo yanalenga kuhimiza utandawazi na maendeleo ya uchumi.

Aidha amesema mada za kongamano hilo ni muhimu katika kutimiza lengo hilo na kongamano hilo litasaidia kuongeza kuvutia uwekezaji barani Afrika.

Rais Denis Sassou Nguesso wa Kongo amesema, uwekezaji kutoka China umechangia sana kwenye maendeleo ya uchumi barani Afrika, na kutaka kuimarisha ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika katika sekta za teknolojia ya kidigitali na ujenzi wa miundo mbinu.

Rais Paul Kagame wa Rwanda akihutubu katika Kongamano la 5 la uwekezaji barani Afrika

Ripoti yenye kauli mbiu ya teknolojia za kidigitali kwa wote barani Afrika, imewasilishwa na Banki ya Dunia katika kongamano hilo ambapo imesisitiza umuhimu wa kuwapa wafanyakazi ujuzi wa kidigitali na kutatua tatizo la kuwa na ujuzi wa kimsingi wa teknolojia za kidigitali.

Kongamano hilo la siku tatu lilianza Jumanne na limeandaliwa kwa pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Kongo, Wizara ya Fedha ya China, Banki ya Maendeleo ya China na Banki ya Dunia.

 

Tags

Maoni