Sep 18, 2019 12:56 UTC
  • Watoto 26 wapoteza maisha Liberia baada ya shule kuteketea moto

Watoto wasiopungua 26 wamepoteza maisha nchini Liberia baada ya shule yao ya bweni kuteketea moto nje ya mji mkuu Monrovia.

Kwa mujibu wa taarifa, watoto walikuwa wamelala wakati shule yao ilipoanza kuteketea Jumanne usiku. Taarifa zinasema shule iliyoteketea moto ilikuwa maalumu ya kufunza Qur'ani Tukufu. Msemaji wa Polisi  ya Liberia Moses Carter amesema bado hawajaweza kubaini chanzo cha moto huo uliojiri katika mji wa Pyanesville. Taarifa zinasema waalimu wawili pia wamepoteza maisha katika tukio hilo la kusikitisha.

Rais George Weah wa Liberia ametuma salamu zake za rambi rambi kufuatia msiba huo na kusema huu ni wakati mgumu kwa taifa la Liberia na familia za waathirika. Aidha Rais Weah ametembelea eneo la maafa na kujiunga na waathirika katika maombolezo.

 

Maoni