Sep 24, 2019 12:12 UTC
  • Wamorocco wakasirishwa na kupeperushwa bendera ya Israel nchini kwao

Safari ya ujumbe wa utawala haramu wa Israel ukiongozwa na mmoja wa viongozi wa chama cha Likud nchini Morocco na kupeperushwa bendera ya utawala huo kusini mashariki mwa nchi hiyo, kumezua malalamiko ya Wamorocco.

Gazeti la Al-Quds Al-Arabi limeripoti kwamba wanaharakati wanaopinga kuboreshwa uhusiano na utawala haramu wa Kizayuni wametoa taarifa inayopinga vikali safari ya ujumbe huo wa Israel ulioongozwa na David Ankava, kibaraka wa Kizayuni, mjumbe wa chama cha Likud na mmoja wa waliogombea kwenye uchaguzi wa bunge ndani ya utawala huo wa Kizayuni. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ankava aliongoza ujumbe wa utalii wa Wazayuni nchini Morocco na kupeperusha bendera ya utawala khabithi wa Kizayuni nchini humo. Aidha taarifa hiyo imeendelea kubainisha kwamba ujumbe huo ulioongozwa na mwanasiasa huyo wa Kizayuni ulijumuisha maafisa wa jeshi, maafisa wa upelelezi na wanasiasa wa Israel, na kongeza kuwa pamoja na kuwa msafara huo ulisharejea Israel lakini ulifanikiwa kutekeleza malengo yake machafu ya kupenyeza zaidi nchini Morocco na kuvutia uungaji mkono katika sehemu tofauti.

Wamorocco wakipinga kupeperushwa bendera ya Israel ndani ya ardhi yao

Kadhalika taarifa ya wanaharakati hao wa Morocco wanaopinga kuboreshwa uhusiano na utawala wa Kizayuni wamemtaja David Ankava, mmoja wa maafisa wa jeshi la Israel na mjumbe wa chama cha Likud kinachoongozwa na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, kuwa amekiuka kwa mara nyingine haki ya kujitawala taifa la Morocco na kutundika bendera ya utawala haramu wa Kizayuni kwenye miinuko ya changarawe kusini mashariki mwa nchi hiyo. Itakumbukwa kuwa mwezi Machi mwaka huu David Ankava alifanya safari nchini Morocco akiwaongoza maafisa wa jeshi la Israel kama ambavyo pia mwezi Oktoba 2011 alilitembelea bunge la nchi hiyo. Mwanasiasa huyo wa Kizayuni anadai kuwa, jumla ya Wazayuni laki nane wanaoishi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, wana asili ya Morocco.

Tags

Maoni