Oct 22, 2019 16:47 UTC

Jamii ya kimataifa imetakiwa kusaidia kuhitimisha mapigano ya wenyewe kwa wenye yaliyoanza mwanzoni mwa mwaka huu katika maeneo ya nyanda za juu mkoa wa Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kupelekea kwa akali watu 500 kuuawa.

Kwa mujibu wa mashuhuda, mauaji hayo yanatekelezwa na wapiganaji wa kundi la Mai-Mai ambalo linaundwa na makundi ya Banyindu, Bafurero, Wabembe na wengine kutokea nchini Burundi.

Askari wa jeshi la serikali ambao wameshindwa kuwamaliza waasi wa Mai-Mai

Hayo yanajiri katika hali ambayo wakazi wa maeneo ya mkoa wa Kivu Kusini wanalishangaa jeshi la serikali kwa kushindwa kuwamaliza wanamgambo hao licha ya kwamba linao uwezo huo. Wakati huo huo nalo jeshi la serikali limeahidi kutuma askari wake katika maeneo hayo ili kuzima mapigano hayo.

Kwa maelezo zaidi tujiunge na mwandishi wa eneo la Afrika ya Kati Mosi Mwasi………………/

 

Tags

Maoni