Oct 23, 2019 07:53 UTC
  • Abiy Ahmed: Ethiopia iko tayari kuendesha uchaguzi 2020

Waziri Mkuu wa Ethiopia jana alisema kuwa nchi hiyo itakabiliwa na matatizo iwapo itachelewesha uchaguzi mkuu kinyume na ilivyopangwa. Uchaguzi mkuu nchini Ethiopia umepangwa kufanyika mwezi ujao wa Mei.

Abiy Ahmed amesema kuwa demokrasia inapaswa kutekelezwa na wanapasa kuwajengea imani wananchi. Waziri Mkuu wa Ethiopia ameongeza kuwa, Tume ya Uchaguzi  inazo fedha na uwezo wa kuendesha zoezi hilo la uchaguzi katika nchi hiyo yenye watu milioni 105. Uchaguzi huo mkuu utakuwa wa kwanza kufanyika Ethiopia chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed aliyeingia madarakani mwezi Aprili mwaka jana na kuanza kutekeleza mageuzi ya kisiasa na kiuchumi.

Ethiopia imekuwa ikiendesha chaguzi mara kwa mara tangu mwaka 1995; lakini machafuko yaliibuka katika uchaguzi wa mwaka 2005 baada ya wapinzani kudai kufanyika udanganyifu, askari usalama kuua waandamanaji karibu 200 waliokuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi na serikali kuwafunga jela wanasiasa wengi wa upinzani.

Ghasia baada ya uchaguzi mkuu nchini Ethiopia mwaka 2005

Waziri Mkuu Abiy Ahmed amesema kuwa, wananchi wa Ethiopia wamepata somo na ibra kutokana na machafuko yote yaliyotokea nchini humo katika uchaguzi wa mwaka 2005. Amesema wananchi hawataki kushuhudia tena ukosefu wa amani unaotokana na uchaguzi.

Tags

Maoni