Oct 23, 2019 07:59 UTC
  • Amnesty International: Uhalifu wa kivita umejiri Tripoli

Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limetanagza kuwa uhalifu wa kivita na ukiukaji wa haki za binadamu umejiri katika mapigano ya kijeshi huko Tripoli mji mkuu wa Libya na viunga vyake.

Shirika la Amnesty International limetangaza katika ripoti yake mpya kuhusu vita huko Tripoli mji mkuu wa Libya kwamba, makumi ya raia wa Libya wamepoteza maisha katika mashambulizi ya kiholela na ya kushtukiza ambapo kulitumiwa silaha za miripuko dhidi ya maeneo ya raia huko Tripoli. 

Wasimamizi wa Amnesty International baada ya kuutembelea mji mkuu Tripoli na viunga vyake ambako yalijiri mashambulizi ya anga na ya nchi kavu wamepata ushahidi unaoonyesha kutekelezwa uhalifu wa kivita ambao kwa kiasi kikubwa unaelekezewa kufanywa na wanamgambo wanaoongozwa na Kamanda Khalifa haftar kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya na pia serikali ya umoja wa kitaifa. 

Wahanga wa mashambulizi katika mji mkuu wa Libya, Tripoli 
 

Amnesty International imeongeza kuwa, mashambulizi hayo tajwa ni ukiukaji wa haki za binadamu na ni uhalifu wa kivita. 

 

Maoni