Nov 13, 2019 15:47 UTC
  • Watu sita wauawa Mtwara, Tanzania, Polisi waanzisha uchunguzi

Polisi nchini Tazania wameanzisha uchunguzi baada ya watu sita kuuawa katika kijiji cha Nongo, Wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtawara.

Kwa mujibu wa taarifa watu saba wamejeruhiwa katika mauaji hayo yaliyojiri usiku wa kuamjia jana Jumanne Novemba 12 katika mpaka wa Tanzania na Msumbuji.

Maafisa wa usalama wanasema raia hao wa Tanzania walipigwa risasi na watu wanaodhaniwa kutoka nchi jirani ya Msumbuji wakati wakiwa visiwa vya Mtor Ruvuma wanakofanya shughuli za kilimo.

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI, Robert Boaz

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI, Robert Boaz amesema hatua madhubuti zitachukuliwa na polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola ili kuhakikisha wote waliohusika na tukio hilo wanapatikana na kuchukuliwa hatua.

 

Tags

Maoni