Nov 16, 2019 06:34 UTC
  • Wanamgambo wa ADF washambulia kijiji na kuua watu kadhaa Kongo DR

Genge moja la wanamgambo limeshambulia kijiji kimoja na kuua watu sita wa familia moja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Duru za kiusalama zimeripoti kuwa, baba na watoto wake watano walipigwa risasi na kuuawa papo hapo na wapiganaji hao wa ADF katika mkoa wa Beni, mashariki wa nchi hiyo Ijumaa. 

Baadhi ya duru habari zinaarifu kuwa, waliouawa katika shambulizi hilo la jana ni watu wanane. Shambulizi hili linaonekana kuwa la ulipizaji kisasi.

Haya yanajiri siku chache baada ya vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutangaza habari ya kuwaangamiza wapiganaji 25 wa kundi hilo la wanamgambo katika mji wa mashariki wa Beni, ulioko katika mkoa wa Kivu Kaskazini. 

Wapiganaji wa ADF wanaotokea Uganda

Aidha jeshi la nchi hiyo lilifanikiwa pia kudhibiti maeneo manne ambayo yalikuwa ngome za wapiganaji hao mkoani Kivu Kaskazini, katika operesheni hiyo iliyoanza tangu Oktoba 30.

Katika miezi ya hivi karibuni, wanamgambo hao wa ADF ambao asili yao ni Uganda wamekuwa wakiwashambulia maafisa wa afya wanaopambana na ugonjwa hatari wa Ebola, mashariki mwa nchi.

Tags

Maoni