Nov 21, 2019 11:58 UTC
  • Polisi ya Sudan yawatia mbaroni viongozi wa chama cha Kongresi ya Wananchi

Jeshi la polisi nchini Sudan limemtia mbaroni Katibu Mkuu wa Chama cha Kongresi ya Wananchi akiwa nyumbani kwake kusini mwa Khartoum, mji mkuu wa nchi hiyo.

Viongozi wa serikali ya mpito nchini Sudan walitangaza jana kwamba Ali al-Haj ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kushiriki katika mapinduzi ya mwaka 1989 nchini Sudan. Kadhalika polisi wa nchi hiyo wamethibitisha habari ya kutiwa mbaroni Ibrahim Al Sinusi, mkuu wa kamati ya Baraza la Chama cha Kongresi ya Wananchi. Chama hicho ni tawi lililojitenga na chama cha Kongresi ya Kitaifa kinachoongozwa na Omar al-Bashir, rais aliyeondolewa madarakani nchini humo.

Mapinduzi ya mwaka 1989 yalimuingiza madarakani Omar al-Bashir

Kabla ya hapo pia kamati ya kisheria ya muungano wa kundi la Uhuru na Mabadiliko nchini Sudan iliiyoongoza maandamano ya hivi karibuni ya wananchi ilimtaka mwendesha mashtaka wa serikali kumtia mbaroni Ali al-Haj na Ibrahim Al Sinusi kutokana na kuhusika kwao katika mapinduzi ya mwaka 1989 ambayo yalimuingiza madarakani Omar al-Bashir. Maandamano ya wananchi nchini Sudan yalianza tarehe 19 Disemba mwaka jana kufuatia kupanda kwa bei ya mkate, hata hivyo maandamano hayo yalishika kasi na kuchukua sura ya kisiasa ambapo matokeo yake yalikuwa ni kung'olewa madarakani Omar al-Bashir.

Tags

Maoni