Dec 08, 2019 11:57 UTC
  • Israel inawapa mafunzo ya kijeshi wapiganaji wa Haftar Libya

Gazeti la Qatar la Al-Araby Al-Jadeed limefichua kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel linawapa mafunzo ya kijeshi wanamgamboa wa kundi la wapiganaji linaloongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar ambalo linajiita Jeshi la Taifa la Libya.

Gazeti hilo limenukuu duru za habari za Misri na Libya zikisema kuwa, vikosi vya Haftar na utawala haramu wa Israel vimeafikiana kuhusu kuimarisha uhusiano wa pande mbili wa kijeshi.

Habari zaidi zinasema kuwa, askari wa jeshi la Israel wanawapa mafunzo maalumu wanamgambo hao wa Khalifa Haftar yanayofahamika kama "Urban Warfare"  ili kuwapa ujuzi wa kuweza kuuteka na kuudhibiti mji mkuu Tripoli.

Mgogoro mpya unaoshuhudiwa Libya hivi sasa ulianza baada ya kundi hilo linalojiita Jeshi la Taifa la Libya, kuanzisha vita vya kila upande mwezi Aprili mwaka huu kwa tamaa ya kuuteka mji mkuu wa nchi hiyo.

Kamanda muasi, Khalifa Haftar akipiga saluti

Hata hivyo waasi hao wameshindwa kuuteka mji huo licha ya kuungwa mkono kikamilifu na Saudi Arabia, Misri, Imarati na baadhi ya nchi za Magharibi ikiwemo Marekani.

Uvamizi huo unaendelea kulaaniwa hadi leo hii na jamii ya kimataifa hasa kwa vile hadi hivi sasa zaidi ya watu 1,090 wameshauawa na 57,000 kujeruhiwa tangu jenerali huyo muasi alipoanzisha vita dhidi ya Tripoli.  

Tags

Maoni