Dec 12, 2019 12:16 UTC
  • Sudan yatajwa kuwa kituo kikubwa kabisa cha Shirika la Ujasusi la Marekani CIA barani Afrika

Katibu Mkuu wa chama cha Kikomunisti nchini Sudan ameikosoa serikali kwa kuridhia ardhi ya nchi hiyo iwe makao ya kituo kikubwa kabisa cha Shirika la Ujasusi la Marekani CIA barani Afrika.

Muhammad Mukhtar al-Khatib, Katibu Mkuu wa chama cha Kikomunisti nchini Sudan amesema katika mahojiano na gazeti la al-Akhbar linalochapishwa nchini Lebanon kwamba, vikosi vya Sudan vinapigana vita kupitia Kamandi Kuu ya Kijeshi ya Marekani Afrika (AFRICOM) kwa ajili ya kulinda maslahi ya Marekani na chini ya amri ya walinzi wa ulinzi wa nchi hiyo.

Al-Khatib ameongezea kwa kusema: "Nchi yetu ni makao ya kituo kikubwa kabisa cha shirika la CIA barani Afrika. Sisi hatupendi ardhi na anga ya nchi yetu viwe chanzo cha ubeberu dhidi ya wengine au chimbuko la maudhi kwa mataifa mengine."

Muhammad Mukhtar al-Khatib

Katika sehemu nyingine ya mahojiano hayo, kiongozi huyo wa chama cha Kikomunisti nchini Sudan amesema, rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir ndiye anayebeba dhima ya kuwepo wanajeshi wa nchi hiyo nchini Yemen na akaongeza kwamba, askari wa Sudan walioko nchini humo wanashiriki kwenye vita ambavyo haviwahusu Wasudani ndewe wala sikio.

Kuanzia tarehe 19 Desemba mwaka uliopita wa 2018 Sudan ilishuhudia maandamano ya upinzani ya wananchi ya kupinga serikali, yaliyofanyika katika mji mkuu Khartoum na miji mingine ya nchi hiyo.

Maandamano hayo yaliyokuwa ya kulalamikia ughali wa bidhaa na hali mbaya ya maisha hatimaye mnamo tarehe 11 Aprili mwaka huu yalipelekea kung'olewa madarakani Omar al-Bashir na kuingia madarakani serikali ya mpito iliyopo hivi sasa.../  

 

Tags

Maoni