Dec 14, 2019 16:34 UTC

Mazungumzo kati ya wajumbe wa Rwanda na Uganda yaliyofanyika jana Ijumaa nchini Uganda yalimalizika bila kufikiwa natija iliyokuwa ikitarajiwa.

Mazungumzo hayo yaliyoitishwa na nchi wapatanishi kwa lengo la kumaliza mzozo uliopo kati ya pande mbili, yalikumbwa na mkwamo baada ya wajumbe wa pande mbili kushindwa kuafikiana kuhusu masuala yenye utata.

Mpaka wa Rwanda na Uganda ambapo wafanyabiashara wa nchi mbili wanataabika sana

Masuala kama vile uwepo wa askari wa Uganda nchini Rwanda pamoja na kukamatwa kinyume cha sheria Wanyarwanda nchini Uganda, ni masuala yaliyojadiliwa kwenye mazungumzo hayo. Mzozo kati ya Rwanda na Uganda uliibukka tapata mwaka mmoja sasa ambapo pande mbili zimekuwa zikirushiana lawama.

Jiunge na mwandishi wetu wa mjini Kampala, Kigozi Ismail kwa kubonyeza alama ya sauti pale juu............/

Tags

Maoni