Dec 15, 2019 01:12 UTC
  • Kundi la Boko Haram laua mateka wanne lililokuwa likiwashikilia Nigeria

Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram, limewaua mateka wake wanne lililokuwa likiwashikilia, ambao ni mfanyakazi wa shirika la kimataifa la misaada ya kibinaadamu nchini Nigeria.

Shirikka la 'Action Against Hunger' limetangaza kwamba kundi hilo la kigaidi limewaua wafanyakazi wake wanne ambao liliwateka nyara mwezi Julai mwaka huu huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Aidha shirika hilo limeongeza kwamba juhudi kubwa kwa ajili ya kuwaachiliwa kwao huru hazikuzaa matunda na hivyo limelaani vikali kitendo hicho cha kuuawa wafanyakazi wake hao. Kwa mujibu wa habari hiyo, wafanyakazi wa shirika hilo la Action Against Hunger walitiwa mbaroni karibu na mji wa Damasak, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Shirika la Action Against Hunger

Kabla ya hapo jeshi la polisi la nchi hiyo lilitangaza kwamba lilifanikiwa kuwaokoa zaidi ya mateka 300 waliokuwa wanashikiliwa na kundi hilo la kigaidi, ambapo wengi wao ni watoto katika jengo moja la mji wa Kaduna, kaskazini mwa Nigeria. Kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa, katika muongo mmoja wa shughuli za kundi la Boko Haram nchini Nigeria, zaidi ya watu elfu 30 wameuawa na wengine wanaokaribia milioni tatu wamekuwa wakimbizi. Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram lilianzisha shughuli zake za kigaidi mwaka 2009 kaskazini mwa Nigeria ambapo hadi sasa limepanua wigo wake hadi katika nchi za Niger, Chad na kaskazini mwa Chad.

Tags

Maoni