Dec 23, 2019 13:26 UTC
  • Sami Anan
    Sami Anan

Sami Anan Mkuu wa zamani wa jeshi la Misri ameachiwa huru kutoka kizuizini ambapo alikuwa akishikiliwa kwa karibu miaka miwili kwa kosa la kutaka kugombea kiti cha rais mwaka uliopita.

Anan ambaye sasa yuko nyumbani kwake alikuwa akizuiwa katika jela ya jeshi hadi pale alipopatwa na kiharusi mwezi Julai mwaka jana na kuhamishiwa katika hospitali ya jeshi katika kitongoji cha Maadi mjini Cairo. Anan alikuwa amelazwa huko hadi alipoachiwa huru jana.

Sami Anan ambaye alitambulika kama mpinzani mkuu wa Abdel Fattah al Sisi katika uchaguzi wa rais wa mwaka jana, alitiwa mbaroni na kuzuiwa kugombea kiti cha urais baada ya jeshi kumtuhumu kwamba, alitaka kuwania kiti cha urais bila ya ruhusa. Jeshi lilisema kuwa hatua hiyo ya Anan ni kinyume na sheria ya jeshi.

Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri alichaguliwa mwa muhula wa pili mwaka jana baada ya kutangazwa kuibuka na ushindi wa asilimia 97 ya kura. Uchaguzi huo ulishirikisha watu milioni 23 kati ya milioni 60 ya waliotimiza masharti ya kupiga kura; kiwango ambacho ni sawa na asilimia 40 ya wapiga kura. Uchaguzi huo aidha ulisusiwa kwa kiasi kikubwa na vyama vikuu vya upinzani.

Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri  

 

Tags

Maoni