Jan 05, 2020 15:29 UTC
  • Kambi ya jeshi la Kenya ambayo wamo askari wa Marekani yashambuliwa

Maafisa usalama nchini Kenya wametangaza kujiri shambulizi dhidi ya kambi ya jeshi la nchi hiyo ambayo wapo askari wa Marekani ndani yake.

Taarifa iliyotolewa leo na maafisa usalama wa Kenya imesema kuwa, kundi moja la wabeba silaha limeshambulia kambi hiyo ya jeshi inayoitwa Kambi Simba. Kwa mujibu wa habari hiyo magaidi wa kundi la ash-Shabab ndio wamehusika na hujuma hiyo  dhidi ya kambi hiyo ambayo ndani yake wapo askari wa Marekani mjini Lamu nchini Kenya na kuisababishia hasara. Maafisa usalama nchini Kenya wameongeza kwamba kumejiri mapigano makali, yaliyomalizika kwa kuwarejesha nyuma wavamizi, ingawa haijaarifiwa iwapo kuna watu waliouawa au kujeruhiwa katika mapigano hayo.

Kambi ya jeshi la Kenya ambayo ndani yake wapo askari wa Marekani

Kundi la kigaidi la ash-Shabab limetoa taarifa ambayo sambamba na kukubali kuhusika na hujuma hiyo, limetangaza kuwa limefanikiwa kuwasababishia hasara kubwa askari wa Marekani na wa Kenya ambao wapo eneo hilo. Habari zinaarifu kuimarishwa usalama baada ya kujiri shambulizi hilo. Kundi la ash-Shabab ambalo makao makuu yake ni nchini Somalia, limekuwa likitekeleza mashambulizi makali ndani ya nchi hiyo ya pembe ya Afrika na hata katika nchi jirani na taifa hilo.

Tags

Maoni