Jan 16, 2020 03:01 UTC
  • Bunge la Kiarabu lamuunga mkono Haftar na kutaka  kuondoka Uturuki huko Libya

Bunge la Kiarabu limewaunga mkono wanamgambo wanaoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar na limetaka kuondoka wanajeshi wa Uturuki huko Libya.

Bunge la Kiarabu lenye makao yake Cairo Misri jana lilifanya kikao kilichojadili kadhia ya Libya na baada ya kumalizika lilitoa taarifa iliyokutaja kuwepo wanajeshi wa Uturuki huko Libya kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa. Aidha lilisema hatua hiyo itashadidisha tu mgogoro wa nchi hiyo. Bunge la Kiarabu limeongeza kuwa mswada uliopasishwa na bunge la Uturuki wa kutumwa wanajeshi wa nchi hiyo huko Libya ni kinyume na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na haukubaliki. Uturuki imetuma wanajeshi wake Libya kufuatia ombi la serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi ya wanamgambo wa Khalifa Haftar katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli. 

Jenerali Khalifa Haftar  

Wanamgambo kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya wanaoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar walianzisha mashambuliz katika mji mkuu huo tangu Aprili mwaka jana kwa uungaji mkono wa Saudi Arabia, Imarati na Misri. Mji mkuu wa Libya Tripoli unadhibitiwa na serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Fayez al Sarraj. 

Tags

Maoni