Feb 05, 2020 14:21 UTC
  • AU yaunga mkono mchakato wa amani wa Sudan Kusini

Umoja wa Afrika AU umeelezea kufurahishwa kakwe na juhudi za kuutafutia ufumbuzi wa kisiasa mgogoro wa Sudan Kusini ambao unalenga kurejesha amani katika nchi hiyo iliyokumbwa na machafuko tangu kuasisiwa kwake.

Katika taarifa yake ya leo Jumatano, Baraza la Usalama na Amani la AU limezitaka pande zote zinazohusika na mgogoro wa Sudan Kusini kuzingatia mambo muhimu ya kurahisisha utekelezaji wa makubaliano ya amani baina ya pande hasimu. 

Baraza hilo limegusia pia kuwepo kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar huko Juba na kumhamasisha ahamie kikamilifu na moja kwa moja katika mji mkuu huo wa Sudan Kusini.

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini (kulia) akipeana mkono na hasimu wake mkubwa Riek Machar

 

Nchi hiyo changa zaidi barani Afrika ilitumbukia kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwezi Disemba 2013 baada ya Rais Salva Kiir wa nchi hiyo kumtuhumu makamu wake wakati huo, Riek Machar kuwa amepanga njama za kumpindua. 

Sudan Kusini ilijitenga na Sudan mwaka 2011 kwa kupiga kura ya maoni iliyoungwa mkono na asilimia 99 ya raia wake baada ya vita vya miongo kadhaa vya kupigania kujitenga. Inasadikiwa kuwa Sudan Kusini ilichochewa na madola ya kibeberu kujitenga na Sudan.

Vita vya ndani nchini humo vilivyoanza Disemba 2013 vimeshababisha mauaji ya maelfu ya watu na kulazimisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi. 

Itakumbukwa pia kuwa Rais Salva Kiir ni kutoka kabila la Dinka huku makamu wake wa zamani, Riek Machar akiwa ametoka kabila la Nuer.

Tags

Maoni