Feb 08, 2020 07:40 UTC
  • UN yatahadharisha kuhusu ongezeko la ghasia nchini Sudan Kusini

Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa imetahadharisha juu ya ongezeko la vitendo vya utumiaji mabavu wa silaha kutokana na kuchelewa kutekelezwa makubaliano ya amani na kuzitia doa sheria za haki za binaadamu nchini Sudan Kusini.

Andrew Clapham Mjumbe wa Kamisheni ya Haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa sambamba na kukosoa ongezeko hilo la utumiaji mabavu wa silaha nchini humo, amesema kuwa hatua hiyo imewalazimisha raia wengi kuwa wakimbizi. Ameongeza kwamba 'Licha ya serikali ya Sudan Kusini kuahidiwa dola milioni 100 kwa ajili ya kusimamia ujenzi wa kambi za wakimbizi, lakini imepatikana nusu tu ya fedha hizo.'

Mahasimu wawili wa Sudan Kusini

Mwaka jana Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan Kusini na Riek Machar, kiongozi wa waasi, walikubaliana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Tarehe 22 ya mwezi huu ndio tarehe iliyoainishwa kwa ajili ya kuundwa serikali hiyo. Ghasia na machafuko nchini Sudan Kusini yaliibuka baada ya Rais Salvakiir kumtuhumu Machar kuwa alikula njama ya kufanya mapinduzi ya kijeshi dhidi yake. Licha ya pande mbili kufanya mazungumzo ya amani, lakini zimekuwa zikikiuka mara kwa mara mapatano ya amani na usitishaji vita baina yao.

Tags

Maoni