Feb 17, 2020 03:32 UTC
  • Umoja wa Mataifa wakosoa ukiukwaji wa vikwazo vya silaha  dhidi ya Libya

Afisa wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya amekosoa ukiukwaji wa vikwazo vya siliha viliyowekwa na umoja huo dhidi ya Libya.

Stephanie T. Williams ambaye ni Naibu Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Libya aliyekuwa akizungumza kwenye Mkutano wa Amani wa Munich huko Ujerumani amezikosoa nchi mbalimbali kwa kukiuka vikwazo vya silaha vilivyowekwa na umoja huo dhidi ya Libya na kusema kuwa, vikwazo hivyo vinakiukwa kutokea angani, nchi kavu na baharini na kwamba wakiukaji wanapaswa kuwajibishwa.

Hata hivyo afisa huyo wa Umoja wa Mataifa hakutaja waziwazi majina ya nchi zinazokiuka vikwazo vya silaha dhidi ya Libya.

Stephanie T. Williams.

Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) Saudi Arabia na Misri zinawasaidia kwa hali na mali wapiganaji wa jenerali muasi, Khalifa Haftar dhidi ya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya inayotambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa. 

Saudi Arabia na Imarati pia zimewaajiri na kuwapa mafunzo mamluki kutoka nchi za Sudan na Chad na kuwatuma Libya kulisaidia kundi la Khalifa Haftar. Imesema askari hao mamluki wanapewa fedha nyingi mkabala wa kulinda visima vya mafuta na kupigana vita dhidi ya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa.  

Tags

Maoni