Feb 18, 2020 13:45 UTC
  • UN; Nchi 4 zinahusika na mashambulizi ya droni ya Haftar huko Libya

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa ametanagza kuwa Misri, Imarati, Jordan na Russia zinahusika katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani ya wanamgambo wanaoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar huko Libya.

Yaqub al Halwi Naibu Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya amewaambia waandishi wa habari waliopo makao makuu ya umoja huo huko New York akizungumza kwa njia ya video kutoka Tripoli kwamba, nchi nne hizo zinamuunga mkono Jenerali Khalifa Haftar kwa kuwapatia silaha wanamgambo kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya zikiwemo ndege zisizo na rubani na kuwasimamia moja kwa moja. 

Jenerali Khalifa Haftar, kiongozi wa wanamgambo kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya 

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa nchi hizo nne zinafahamu vyema kuwa utumiaji wa ndege hizo zisizo na rubani si tu kuwa unazilenga taasisi za kijeshi bali mashambulizi dhidi ya raia na taasisi za kiraia kama shule na hospitali na unasababisha hasara na maafa makubwa; ambayo yote ni jinai za kivita.  

Al Halwi amesema kuwa hasara iliyoipata Libya kutokana na kusitishwa uuzaji nje mafuta ya nchi hiyo katika kipindi cha wiki tatu zilizopita imefika zaidi ya dola bilioni moja. 

Naibu Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Libya ameendelea kubainisha kuwa katika zaidi ya miaka 31 ya kuhudumu kwake ndani ya umoja huo hajawahi kushuhudia hali ngumu kama hiyo katika utoaji wa huduma za kibinadamu kwa raia na wakimbizi.

Tags

Maoni