Mar 17, 2020 17:17 UTC

Serikali ya Tanzania imesema shule zote za awali, msingi na sekondari zitafungwa kwa siku 30 kuanzia leo Jumanne Machi 17, ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona (CODIV-19) ndani ya nchi hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumanne, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam.

Juhudi za kukabiliana na virusi vya Corona kila mahali duniani

Amesema wanafunzi wa kidato cha sita walipaswa kuanza mitihani Mei 4, 2020 lakini nao pia watapaswa kusubiri wizara ifanye utaratibu mwingine kulingana na matokeo ya hali ya maambukizi ya virusi vya corona.

Kwa maelezo zaidi tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam, Ammar Dachi……/

Tags

Maoni