Mar 19, 2020 16:41 UTC

Serikali ya Rwanda imepiga marufuku ya siku 30 kwa safari zote za ndege zinazoingia au kutoka nchini humo katika juhuzi za kukabiliana na virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa marufuku hiyo, agizo hilo litaanza kutekelezwa Ijumaa kesho tarehe 20 Machi 2020 kuanzia majira ya saa sita za usiku. Aidha serikali imesema kwamba ndege za mizigo na zile za dharura zitaendelea na safari zao kamakawaida kwa kuingia au kutoka Rwanda.

Ulimwengu uliogubikwa na kirusi cha Corona

Wakati huo serikali ya Rwanda imetangaza ongezeko la waathirika wa virus vya Ccorona kutoka watu wanane siku ya Jumanne na kufikia watu 11 Alkhamisi ya leo.

Bonyeza alama ya sauti pale juu ili kusikiliza ripoti kamili ya mwandishi wetu Sylivanus Karemera kutoka mjini Kigali, Rwanda..……../

Tags

Maoni