Mar 23, 2020 16:26 UTC

Shirika la Kimataifa la International Crisis Group limechapisha taarifa inayohusu hali ya kisiasa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hali ya mambo nchini humo bado ni mbaya sana licha ya kupita mwaka mmoja tangu serikali na makundi 14 yanayobeba silaha kutiliana saini mkataba wa amani baina yao. Aidha shirika hilo limefafanua kuwa, hali hiyo inaweza kuzuia kufanyika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Rais Faustin-Archange Touadéra

Katika sehemu nyingine shirika la International Crisis Group limeikosoa serikali ya Rais Faustin-Archange Touadéra kwa kuzuia mikutano ya makundi ya upinzani na kusisitiza kuwa zuia hilo linabainisha uwepo wa njama za kuchakachua matokeo ya uchaguzi ujao kwa maslahi ya chama tawala.

Jiunge na mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya Kati Mosi Mwasi kwa kubonyeza alama ya sauti pale juu …………../

 

Maoni