Mar 23, 2020 16:37 UTC

Watu sita wenye uraia wa China wametiwa mbano nchini Uganda, wakati wakijaribu kutoroka kutoka nchi hiyo mwakachana wa Jumuisha ya Afrika Mashariki.

Wachina hao waliokuwa wamewekwa karantini, wametiwa mbaroni katika wilaya ya Zombo, iliyo kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa mujibu wa habari kutoka Uganda, Wachina hao walikuwa tayari wametimiza siku 10 katika kizuizi (karantini), huku wakiwa wamebakisha siku nne pekee kumalizi karantini hiyo.

Rais Yoweri Museven wa Uganda

Sasa watapandishwa mahkamani kujibu tuhuma za kukaidi amri ya Rais Museven, ya kuzuia kutoka au kuingia nchi hiyo wakati huu wa kukabiliana na virusi vya Corona hadi pale kutakapotolewa amri nyingine na serikali.

Kwa maelezo zaidi jiunge na mwandishi wetu wa mjini Kampala, Kigozi Ismail kwa kubonyeza alama ya sauti pale juu………………/

 

Tags

Maoni