Apr 08, 2020 16:38 UTC
  • Umoja wa Afrika waliunga mkono Shirika la Afya Duniani (WHO) katika kukabiliana na tuhuma chafu za Trump

Kamisheni ya Umoja wa Afrika imetangaza uungaji mkono wake kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) katika kukabiliana na tuhuma zisizo na msingi za Rais Donald Trump wa Marekani.

Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ametoa radiamali yake kufuatia matamshi ya tuhuma za Trump kulilenga shirika hilo la afya kwamba linaipendelea China. Kupitia ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter Moussa Faki ameandika kuwa, Umoja wa Afrika unamuunga mkono kikamilifu Tedros Adhanom, Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Kadhalika Mwenyekiti huyo wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ametaka ushirikiano zaidi wa kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na virusi vya Corona na kwamba, jamii ya kimataifa ni lazima ijikite kwa namna ya pamoja katika mapambano ya ugonjwa wa Covid-19.

Rais Donald Trump wa Marekani ambaye virusi vya Corona vimemfanya achanganyikiwe na kujikuta akitoa tuhuma hivyo

Radiamali ya  Moussa Faki Mahamat imetolewa baada ya Rais Donald Trump wa Marekani Jumanne ya jana kulituhumuu Shirika la Afya Duniani (WHO) kwamba linaipendelea China na kutishia kuwa huwenda Washington ikalikatia misaada yake ya kifedha shirika hilo. Kadhalika rais huyo wa Marekani alidai kuwa, shirika hilo lina mwelekeo wa China na kwamba lilichelewa hata kutangaza hatari ya kuenea virusi vya Corona. Kabla ya hapo na mwanzoni mwa kuenea virusi vya Corona ambapo viongozi wa Marekani hawakudhani kuwa hali ya mambo nchini Marekani itakuja kuwa mbaya kuliko nchi nyingine za dunia, kiasi cha kufikia kuomba msaada kutoka kwa China, walikuwa wakiichafua nchi hiyo ya Asia (China) kwa kuvitaja virusi hivyo kwa jina la 'virusi vya China' au 'virusi vya Wuhan' suala ambalo lilikosolewa vikali na serikali ya Beijing.

Maoni