May 11, 2020 14:49 UTC

Uchaguzi wa urais, bunge na madiwani wa tarehe 20 ya mwezi huu nchini Burundi huenda utafanyika bila kuwepo waangalizi kutoka nje ya nchi.

Hayo ni baada ya waangalizi wa EAC walotarajiwa kuwasili Burundi kwa ajili ya kufuatilia uchaguzi huo kutakiwa na Tume ya Uchaguzi CENI kufikia karantini kwa muda wa siku 14.

Wafuasi wa chama tawala katika harakati zao kuelekea uchaguzi wa Mei 20

Hii ni katika hali ambayo hadi sasa  zimesalia siku tisa pekee kabla ya kufanyika kwa uchagusi huo.

Tujiunge na mwandishi wetu wa mjini Bujumbura, Hamida Issa kwa taarifa zaidi………/

 

 

Tags

Maoni