May 18, 2020 15:35 UTC

Waislamu wamehimizwa kuendeleza ibada mbalimbali ndani ya kumi la mwisho la mwezi huu wa Ramadhani ili kuweza kupata fadhila za Usiku wa Heshima (Lailatul-Qadr).

Hayo yamesisitizwa na mashekh tofauti visiwani Zanzibar ambao wamewataka Waislamu kuachana na ile dhana kwamba maana ya kudiriki usiku wa Lailatul-Qadr ni kuona nyota kubwa angani, jambo ambalo halina ukweli wowote.

Waumini wa dini ya Kiislamu visiwani Zanzibar kabla ya kuibuka kwa virusi vya Corona

Aidha tukiwa mwishoni mwa mwezi huu wa Ramadhani, kumetolewa nasaha kwamba badala ya kujikita katika manunuzi ya nguo za sikukuu, watu wanatakiwa kutumia fursa hii kujipinda katika ibada na kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu. Ramadhani ya mwaka huu visiwani Zanzibar ilishuhudia darsa hafifu misikitini, kutokana na masheikh kutekeleza maelekezo ya afya ya kukabiliana na virusi hatari vya Corona.

Mwandishi wetu wa visiwani Zanzibar, Harith Subeit anaripoti zaidi………………../

 

Tags

Maoni