May 19, 2020 16:40 UTC

Huku ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na virusi vya Corona ukiendelea kuwakumba na kuwawafanya watu wengi kuwa wahanga, kumeendelea pia kushuhudiwa juhudi za kukabiliana na janga hilo.

Katika uwanja huo, watu mbalimbali wamejitokeza na kudai kupata dawa ya kukabiliana na ugonjwa huo. Hii ni katika hali ambayo mashirika ya afya hayajaunga mkono dawa hizo na hivyo kuendelea kuwa kitendawili juu ya usahihi wa dawa zinazotangazwa. Nchini Cameroon amejitokeza mtu ambaye amedai kuunda dawa ya Corona ambayo amedai kuweza kuwatibu watu wengi.

Tujiunge na mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya Kati Mosi Mwasi ambaye ametuandalia taarifa ifuatayo kuhusiana na suala hilo……../

 

Maoni