May 21, 2020 15:37 UTC

Hatimaye bunge la Ufaransa limepitisha sheria ya kuondoa udhibiti wake kwenye fedha za CFA ambazo zilikuwa zikitumika katika makoloni yake ya zamani ya Afrika Magharibi.

Ufaransa imechukua hatua hiyo kwa lengo la kuanzisha fedha nyingine itakayoitwa ECO ambayo kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Paris na makoloni yake hayo ya Afrika Magharibi, Ufaransa haitakuwa na udhibiti wowote kwenye fedha hiyo mpya.

Makubaliano ya kufutwa fedha hiyo yalifikiwa kati ya Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast  na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa

Hata hivyo nchi ambazo hazikuwahi kuwa makoloni ya Ufaransa na ambazo nazo zinatumia fedha ya CFA, zimetilia shaka nia hiyo ya Ufaransa, ambapo zimeitaja kuwa ni njama za Paris za kutaka kujipenyeza zaidi ndani ya mataifa hayo. Fedha za CFA zilianza kutumika tangu mwaka 1937 huku Ufaransa ikiwa ndio mnufaika mkuu wa fedha hizo kinyume na walengwa wenyewe wa Kiafrika.

Mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya Kati Mosi Mwasi ametuandalia taarifa ifuatayo………………./

 

 

Maoni