May 21, 2020 15:38 UTC

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ya Rwanda amesema kuwa baada ya kumtia mbaroni mshukiwa mkuu wa mauaji ya kimbari ya nchi hiyo ya mwaka 1994, bwana Felician Kabuga, msako unaendelea.

Kwa mujibu wa Aimable Havugiyaremye vinara wote waliopanga na kutekeleza mauaji hayo na ambao bado wameendelea kuishi kwa uficho katika mataifa mbalimbali ya dunia, watasakwa kwa njia yoyote na hatimaye warushwe nchini Rwanda ili wakajibu tuhuma zinazowahusu.

Aimable Havugiyaremye, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Rwanda

Aidha Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Rwanda amebainisha kuwa, serikali ya Kigali imekuwa ikikabiliwa na kizuizi cha kuwarejesha nchini washukiwa hao wa mauaji kutokana na baadhi ya watuhumiwa hao kubadili uraia wa nchi wanazoishi, sambamba na kuwepo usiasa mwingi badala ya kufuatwa kwa sheria.

Tujiunge na mwandishi wetu wa mjini Kigali, Sylivanus Karemera kwa ripoti zaidi…………

Tags

Maoni