May 22, 2020 07:59 UTC
  • Wataalamu waonya; huenda corona ikaua 50,000 nchini Afrika Kusini

Wanasayansi wametahadharidha kuwa, huenda vifo vya ugonjwa wa Covid-19 nchini Afrika Kusini vikapindukia 50,000 kufikia mwishoni mwa mwaka huu 2020.

Utafiti uliofanywa na wanasayansi hao kwa niaba ya Wizara ya Afya ya Afrika Kusini unatabiri kuwa, huenda nchi hiyo ikashuhudia vifo vya Corona baina ya 35,000 na 50,000 kufikia mwezi Novemba mwaka huu, mbali na wengine zaidi ya milioni 3 kuambukizwa virusi vya corona, kwa kuwa virusi hivyo husambaa kwa kasi zaidi katika msimu wa baridi kali.

Afrika Kusini ambayo imerekodi kesi 18,000 za watu walioambukizwa virusi vya Corona na vifo zaidi ya 330 vya ugonjwa huo hadi saa, inaongoza kwa idadi ya maambukizi na vifo barani Afrika.

Walioambukizwa corona kote dunia wakaribia milioni 2

Kwa mujibu wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC), idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika imepindukia elfu 95, huku idadi ya vifo ikiongezeka na kufikia 2,997 hadi sasa.

Mbali na Afrika Kusini, nchi nyingine za Afrika zilizoathiri zaidi ya ugonjwa wa Covid-19 ni Misri, Algeria na Morocco. Hivi karibuni, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa utabiri likisema kuwa robo moja ya jamii ya watu bilioni moja barani Afrika, itapatwa na virusi vya Corona kufikia mwaka ujao wa 2021.

Tags

Maoni