May 23, 2020 08:02 UTC
  • Polisi ya Burundi yawakamata mamia ya waangalizi wa uchaguzi

Polisi nchini Burundi imewatia mbaroni mamia ya waangalizi wa uchaguzi wa upinzani, waliokuwa wakifuatilia uchaguzi mkuu uliofanyika siku chache zilizopita.

Msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha National Freedom Council (CNL) ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, mamia ya maafisa wa timu ya uangalizi wa uchaguzi ya upinzani wamekatwa na maafisa usalama nchini humo.

Terence Manirambona amesema, "uchaguzi ulizungukwa na vitisho, kasoro za hapa na pale, wangaalizi 200 wa CNL walitiwa mbaroni, huku baadhi ya watu wakipiga kura mara kadhaa wakitumia majina ya watu waliokufa, wakimbizi na wafungwa."

Haya yanajiri huku wananchi wa Burundi wakisubiri kwa hamu na shauku kuu matokeo ya uchaguzi huo mkuu uliofanyika Jumatano iliyopita. Matokeo hayo yanapaswa kutangaza ndani ya wiki moja baada ya zoezi hilo.

Katika uchaguzi wa rais, iwapo hakuna mgombea atapata asilimia 50 ya kura, uchaguzi huo utaingia katika duru ya pili katika kipindi cha wiki mbili zijazo. 

Wagombea wakuu wa uchaguzi wa rais Burundi

Kuna wagombea saba waliojitokeza kuwania nafasi ya urais, lakini ni wawili tu ndio wanaobashiriwa kuwa na uwezekano wa kuchaguliwa, kurithi mikoba ya Pierre Nkurunziza ambaye yuko madarakani kwa miaka 15.

Wagombea hao ni Evariste Ndayishimiye, Katibu Mkuu wa chama tawala nchini humo cha CNDD-FDD, na Agathon Rwasa, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha CNL.

 

Tags

Maoni