Jun 01, 2020 07:35 UTC
  • Hali ya maambukizi ya corona nchini Senegal inatia wasiwasi

Hali ya maambukizi ya virusi vya corona nchini Senegal khususan katika mji mkuu wa nchi hiyo imewapelekea maafisa wa afya na tiba wa nchi hiyo kubainisha wasiwasi wao.

Televisheni ya France 24 imeripoti kuwa Abdoulaye Diouf Sarr Waziri wa Afya wa Senegal jana alieleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu hali ya mji mkuu Dakar. Hadi sasa watu 3,645 wameambukizwa corona huko Senegal na 4 wameaga dunia. Zaidi ya nusu ya watu walioambukizwa virusi vya corona wameripotiwa katika mji mkuu Dakar.  

Abdoulaye Diouf Sarr, Waziri wa Afya wa Senegal 

Hii ni katika hali ambayo jana Jumapili kesi mpya 84 za maambukizi ya corona zilisajiliwa katika mji mkuu huo. Wziara ya Afya ya Senegal inatazamiwa kuchukua hatua mpya za kukabiliana na wimbi la maambukizi katika mji mkuu wa nchi hiyo. Kitambo nyuma Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitahadharisha kuhusu taathira za maambukizi ya corona barani Afrika kutoka na kukosekana miundomsingi ya afya.   

Takwimu mpya zinaonyesha kuwa hadi sasa watu zaidi ya milioni 6, laki moja na elfu 85 wameambukizwa virusi vya corona duniani; huku watu zaidi ya milioni mbili na laki saba na elfu 54 wakipata nafuu na kuruhusiwa kutoka hospitali. Aidha zaidi ya watu 371,000 wameaga dunia kwa ugonjwa wa Covid-19.

Tags