Jul 03, 2020 12:56 UTC
  • KEMRI: Wakenya zaidi ya milioni 2.5 wameugua ugonjwa wa COVID-19

Wanasayansi nchini Kenya wameeleza baada ya kupima damu iliyotolewa kwa ajili ya protini inayotumika kwenye mfumo kinga kwamba, karibu Wakenya milioni 2.6 tayari wana virusi vya corona.

Protini hiyo (antibody) hutengenezwa na mwili kwa ajili ya kushambulia virusi na bakteria, na uwepo wake kwenye damu unaashiria kuwa mtu huyo hakuwahi kuwa na maambukizi hata kama mtu huyo hakuwahi kuonesha dalili.

Watafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa tiba nchini Kenya wameunga mkono mfuko wa kuchangia damu uliofanyika nchi nzima kati ya mwezi Aprili tarehe 30 na tarehe 16 Juni.

''Kupimwa kwa antibodies kumeonesha kuwa, Wakenya wengi tayari wamepata maambukizi kuliko ilivyokuwa ikibainika katika shughuli za upimaji nchini humo.,'' Ilieleza taasisi ya Kemri mapema wiki hii.

Kemri inakadiria kuwa karibu watu 550,000 jijini Nairobi na karibu 100,000 mjini Mombasa, tayari wameugua virusi hivyo na kupona na pengine kupata kinga.

Imeelezwa kuwa baadhi inawezekana waliathirika mapema mwezi Machi kwa kuwa protini hizo zinazopambana na virusi zinaweza kuwa kwenye damu kwa miezi kadhaa.

Idadi hiyo inaonesha kuwa Wakenya wameshuhudia idadi kubwa ya watu waliopata maambukizi halikadhalika vifo, taasisi hiyo ya utafiti ikikisia kuwa takriban watu 6,000 watakuwa wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Covid-19 nchi nzima, kutokana na idadi ya sasa ya vifo nchini humo kwa ujumla.

 

 

Maoni