Jul 13, 2020 13:02 UTC
  • Andry Rajoelina
    Andry Rajoelina

Wabunge wawili, seneta mmoja na naibu seneta wa Madagascar wameaga dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Habari hiyo imetangazwa na Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina.

Rais wa Madagascar ameongeza kuwa, maseneta wengine 14 na manaibu wao 11 wamepatikana na virusi vya corona vinavyoendelea kuua maelfu ya watu katika pembe mbalimbali za dunia.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni serikali ya Madagascar ilianza kutekeleza tena baadhi ya sheria kali za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona zilizokuwa zimesimamishwa ikiwa ni pamoja na kufunga mji mkuu wa nchi hiyo, Antananarivo kutokana na kuongezeka kwa kasi maambukizi mapya.

Zaidi ya visa 5,080 vya maambukizi ya corona vimeripotiwa nchini Madagascar na watu wasiopungua 37 wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo.

Rais wa Madagascar akitumia dawa iliyodaiwa kutibu corona

Kabla ya mlipuko wa sasa wa corona nchini Madagascar, serikali ya nchi hiyo ilikuwa ikisambaza dawa asili katika baadhi ya nchi za Afrika ikidai kuwa inasaidia watu waliopatwa na virusi hivyo. Dawa hiyo haijathibitishwa na chombo chochote cha kujitegemea.

Tags

Maoni