Jul 30, 2020 10:43 UTC
  • UN: Raia milioni 1.8 waliopoteza makazi yao Nigeria  wanahitaji ulinzi

Umoja wa Mataifa umebainisha wasi wasi wake kuhusu usalama wa watu milioni 1.8 waliopoteza makazi yao nchini Nigeria huku ukosefu wa usalama ukiongezeka kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Farhan Haq, naibu msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuna wasiwasi mkubwa kuhusu ukosefu wa usalama kaskazini mwa Nigeria na jambo hilo linaweza kuathiri utoaji misaaada. Ameashiria tuikio la wafanyakazi watatu wa kutoa misaada kupoteza maisha wakati helikopta ya Umoja wa Mataifa ilipofyatuliwa risasi katika jimbo la Borno, kaskazini mwa Nigeria mapema mwezi huu.

Haq amesema baada ya mapambano kati ya makundi yenye silaha na jeshi la serikali, watu zaidi ya elfu 40 wamepoteza makazi na kukimbilia kwenye kambi ya wakimbizi ambayo imejaa watu mwezi Mei na Juni hukokatika  Majimbo ya Borno, Adamawa na Yobe.

Amesema Umoja wa Mataifa umepokea ripoti za ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa na sheria za haki za binadamu kaskazini mwa Nigeria.

Aidha amesema janga la COVID-19 limepelekea hali iwe mbaya zaidi kote kaskazini mashariki mwa Nigeria ambapo sasa watu milioni 10.6 katika eneo hilo wanahitaji msaada.

Ni zaidi ya muongo mmoja sasa ambapo, eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria limekuwa uwanja wa mashambulizi ya wafuasi wa kundi la kigaidi la Boko Haram.

Zaidi ya watu elfu 30 wameuawa na wengine wanaokaribia milioni tatu wamelazimishwa kuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi ya kundi hilo la Boko Haram nchini Nigeria tokea mwaka 2009. Magaidi hao wakufurishaji pia wamekuwa wakitekeleza mashambulizi katika nchi jirani za Chad, Niger na Cameroon.

 

Tags

Maoni