Aug 02, 2020 09:24 UTC
  • Zoezi la kupiga kura uchaguzi mkuu Zanzibar kufanyika siku mbili

Wananchi wa visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania wanatarajiwa kupiga kura kwa siku mbili katika uchaguzi mkuu utakafanyika Oktoba mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema wananchi wote watapiga kura ya Oktoba 28, lakini siku moja kabla, Oktoba 27, kutakuwa na zoezi la kupiga kura ya mepema ambayo itahusisha makundi yote yatakayohusika kusimia uchaguzi wa Oktoba 28.

Kwa mujibu wa kifungu cha 82 cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2018, upigaji kura ya mapema utawahusu watendaji wanosimamia majukumu ya uchaguzi siku ya uchaguzi.

ZEC imesema uchukuaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa ngazi ya Urais, Uwakilishi na Udiwani utakuwa kati ya Agosti 26 na Septemba 9, na uteuzi utakuwa Septemba 10 mwaka huu.

Vyama vya siasa visiwani Zanzibar vimetangaza kuwa vipo tayari kwa uchaguzi mkuu na kwamba vimekamilisha maandaizi yanayohitajika.

Uchaguzi mkuu Tanzania kufanyika Oktoba mwaka huu.

Watanzania, Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 watafanya uchaguzi mkuu kwa kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge pamoja na Madiwani. Kampeni za uchaguzi mkuu zitaanza rasmi tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020, huku tarehe ya uchaguzi ikianguakia siku ya jumatano ambayo ni tarehe 28 Oktoba 2020.

Tags

Maoni