Aug 05, 2020 11:13 UTC
  • Majaji DRC wapinga sera za mageuzi za Rais Tshisekedi

Majaji wawili katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamepinga mpango wa rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi wa kufanya mageuzi katika mfumo wa mahakama na kuhamishiwa mamlaka katika mahakama ya juu.

Kwa mujibu wa taarifa, majaji hao ni Noel Kilomba na Jean Ubulu kutoka muungano wa wanasiasa unaoungwa mkono na rais wa zamani wa taifa hilo Joseph Kabila.

Majaji hao  hawakuonekana wakati wa sherehe za kuapishwa kwa mawakili na majaji mbele ya Rais Félix Tshisekedi hapo jana Jumanne.

Mbali na majaji hao, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Spika wa bunge la kitaifa na kiongozi wa Senati pamoja na baadhi ya maafisa wa serikali, hawakukubali kushiriki kuapishwa kwa majaji hao wapya, kitendo ambacho kimetafsiriwa na upande wa chama cha UDPS kama kupinga maagizo ya rais.

Joseph Kabila

Vuguvugu la FCC la Joseph Kabila ambalo linao wingi wa viti bungeni, kwenye baraza la seneti limesema kwamba Rais Tshisekedi na wafuasi wake wamekuwa wakiwandama baadhi ya maafisa wa zamani wa serikali, huku wafuasi wa Tshisekedi wakielezea kwamba mawaziri kutoka chama cha Kabila hawawajibiki vyema katika kazi yao.

 

Tags

Maoni