Aug 13, 2020 03:41 UTC
  • Tetemeko kubwa la ardhi laitikisa Tanzania

Tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 6.0 katika kipimo cha limeitikisa Tanzania Jumatano usiku hasa, hasa jiji la Dar es Salaam na maeneo ya Mkoa wa Pwani na Zanzibar na kuibua wahka na taharuki miongoni mwa wananchi.

Taarifa zinasema tetemeko lilijiri  saa 2:13  usiku wa Jumatano na limehisika pia katika nchi jirani ya Kenya.

Kwa mujibu wa tovuti ya volcanodiscovery, kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa kilomita 82 kusini mashariki mwa Dar es Salaam katika Bahari ya Hindi na kina chake kilikuwa ni takribani kilomita 25

Mtetemeko mkubwa kama huo haujawahi kujiri Afrika Mashariki katika miaka ya hivi karibuni kwani eneo hilo liko mbali na maeneo ambayo hukumbwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi mara kwa mara. Hadi sasa hakuna taarifa kamili kuhusu maafa yaliyosababishwa na mtetemeko huo mkubwa wa ardhi.

Mnamo Septemba 2016, tetemeko lililokuwa na ukubwa wa 5.7 katika kipimo cha rishta lilijiri katika eneo la kaskazini magharibi mwa Tanzania na kuua watu 13 na kuwajeruhi wengine 200.