Aug 14, 2020 07:55 UTC
  • Makamu wa rais wa Liberia aambukizwa COVID-19

Makamu wa rais wa Liberia Jewell Taylor ameambukizwa ugonjwa wa COVID-19 au corona na kukimbizwa nchi jirani ya Ghana kupata matibabu.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Liberia inasema Taylor alipimwa virusi hivyo tarehe 10, na matokeo yamethibisha ameambukizwa virusi hivyo.

Taylor alikwenda hospitali iliyo kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Monrovia tarehe 7 kutokana na tatizo la kushindwa kupumua. Baada ya kuthibitishwa kuwa na virusi vya Corona, alihamishiwa katika hospitali ya mji mkuu wa Ghana, Accra, ili kupata matibabu zaidi.

Makamu wa Rais wa Liberia Jewel Howard-Taylor aliyeambukizwa corona amekuwa mstari wa mbele wa kuelimisha jamii kuhusu jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huo

Taylor amekuwa akiongoza kampeni ya kuwataka Waliberia wavae barakoa ili kuzuia kuenea corona. Hadi kufikia sasa watu 1,252 wameambukizwa corona nchini Liberia na 82 miongoni mwao wamefariki dunia.

Wananchi wa Liberia wamekasirishwa na hatua ya viongozi wa nchi hiyo ya kuenda nje ya nchi kupata matibabu hasa katika kipindi hiki cha corona. Mfumo wa Kiafya nchini Liberia haujapewa umuhimu mkubwa na serikali ya sasa na iliyopita ya nchi hiyo baada ya kumalizika vita vya ndani mwaka 2003.

Tags

Maoni