Sep 10, 2020 01:23 UTC
  • Kamati ya pande nne ya Kiarabu yarudia madai yake ya kila siku dhidi ya Iran

Kamati ya pande nne ya nchi za Kiarabu kwa mara nyingine tena imerudia madai yake ya kila siku na yasiyo na msingi wowote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pambizoni mwa kikao cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League).

Kamati hiyo ya pande nne ya Kiarabu inayoongozwa na Imarati na ambayo wanachama wake ni Misri, Saudi Arabia, Bahrain na Katibu Mkuu wa Arab League jana Jumatano iliitisha kikao kwa njia ya Intaneti na kurudia kutoa madai yake ya siku zote na yasiyo na msingi kwamba eti Iran inaingilia masuala ya ndani ya nchi za Kiarabu na kulaani suala hilo. Pande nne hizo za Kiarabu eti zimeitaka Iran iache kuingilia masuala ya ndani ya nchi za Kiarabu na kuzusha hitilafu.  

Madai hayo yasiyo na msingi yametolewa katika hali ambayo nchi hizo hususan Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na Saudi Arabia zenyewe zinaingilia pakubwa masuala ya ndani ya nchi za Kiarabu hususan huko Libya na Yemen. 

Uvamizi wa Saudia na waitifaki wake huko Yemen 

Kamati ya pande nne ya nchi za Kiarabu imetoa taarifa mwishoni mwa kikao hicho na huku ikitilia mkazo suala hilo kwa mara nyingine tena imeitolea wito jamii ya kimataifa kuchukua msimamo madhubuti ili kukabiliana na kile ilichokitaja kuwa ni uzushaji migogoro eti unaofanywa na Iran katika eneo hili.

Tags