Sep 20, 2020 03:15 UTC
  • Ethiopia imemfungulia mashtaka ya ugaidi  Jawar Mohammed na wanaharakati wengine

Ethiopia imewasilisha mashtaka ya ugaidi dhidi ya Jawar Mohammed kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo na wanaharakati wengine; hatua ambayo huwenda ikachochea zaidi machafuko katika eneo la Oromo nchin humo.

Mashtaka hayo yanahusiana na machafuko makubwa yaliyojiri mwezi Julai baada ya kuuliwa Hachalu Hundessa mwimbaji mashuhuri na aliyekuwa mwanaharakati mtajika katika maandamano dhidi ya serikali yaliyompelekea Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuingia madarakani mwaka 2018.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed 

Maafisa wa Ethiopia wamesema kuwa watu zaidi ya 180 waliuawa kwenye machafuko hayo. Mbali na mashtaka hayo dhidi ya Jawar Mohamed, ofisi ya mwanasheria mkuu wa Ethiopia imetangaza pia kuwasilisha mashtaka dhidi ya  washukiwa wengine zaidi ya 20 akiwemo kiongozi wa upinzani wa Oromo Bekele Garba.  Mashtaka hayo yanajumuisha vitendo vya kujaribu kuchochea  machafuko ya kikabila na kidini ili kuwagombanisha raia. Kati ya washukiwa wengine wapo pia wakosoaji wakubwa wa Waziri Mkuu wa Ethiopia wanaoishi nje ya nchi kama mwanaharakati mtajika wa eneo la Oromo, Tsegaye Ragassa na Birhanemeskel Abebe muitifaki wa zamani wa Abiy Ahmed ambaye sasa amekuwa mkosoaji wa serikali. 

Washukiwa hao wanatazamiwa kufika mahakamani kesho Jumatatu.  

Tags

Maoni