Sep 22, 2020 11:45 UTC
  • Rais wa Tunisia ahimiza kulindwa ipasavyo haki za Wapalestina

Rais wa Tunisia ametoa mwito kwa walimwenguni kushirikiana kuhakikisha kuwa Wapalestina wanakombolewa kutoka kwenye makucha ya utawala wa Kizayuni na wanapata haki zao.

Televisheni ya al Jazeera ya Qatar imemnukuu Rais Kais Saied wa Tunisia akitoa mwito huo wakati akihutubia Mkutano Mkuu wa 75 wa Umoja wa Mataifa kwa njia ya video na kusisitiza kuwa, wakati umefika kwa mataifa ya dunia kuwa na fikra moja na kushirikiana katika kukabiliana na dhulma na kulinda haki za mataifa yanayodhulumiwa popote pale ulimwenguni.

Amesema, dunia leo hii inahitajia kuweko Umoja wa Mataifa na ushirikiano katika kutekeleza kivitendo hati na malengo ya kuundwa umoja huo.

Dunia iungane kuikomboa Palestina

 

Rais huyo wa Tunisia amesema pia kwamba, katika miaka na miongo ijayo dunia itashuhudia mabadiliko mengi, hivyo ameyataka mataifa ya dunia kushirikiana kupitia Umoja wa Mataifa na taasisi zake mbalimbali, kuunda historia mpya ya mwanadamu.

Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na utawala wa kiimla wa Bahrain zimetangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusaliti malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina.

Njama za tawala za kidikteta za Kiarabu za kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni zinafanyika katika hali ambayo kwa miaka mingi Wazayuni wanawakandamiza vibaya Wapalestina na wanafanya jinai za kila nui katika maeneo mbalimbali ya Kiarabu na Kiislamu.

Tags

Maoni