Sep 27, 2020 08:02 UTC
  • Wanajeshi wa Kenya na Somalia washambuliana kwa risasi mpakani

Wanajeshi wa Kenya na Somalia wamekabiliana kwa risasi katika mpaka wa pamoja wa nchi mbili hizo jirani za Afrika Mashariki.

Vyanzo vya habari vimelidokeza shirika la habari la AFP kuwa, makabiliano hayo ya risasi yalijiri jana Jumamosi katika eneo la mpakani linaloutenganisha mji wa Bula Hawo wa Somalia na mji wa Mandera ulioko kaskazini mwa Kenya.

Habari zaidi zinasema kuwa, mapamabano hayo ya risasi baina ya askari wa Somalia na Kenya yalianza baada ya kundi la raia wa Somalia waliokuwa na ghadhabu kuandamana wakielekea katika kituo cha mpakani kinacholindwa na wanajeshi wa Kenya.

Inaarifiwa kuwa, raia hao wa Somalia walifanya maandamano hayo kulalamikia mauaji ya wenzao watatu, wanaodaiwa kuuawa na wanajeshi wa Kenya katika mpaka wa nchi mbili hizo.

Kenya na Somalia zimekuwa zikizozana juu ya mpiaka yao ya pamoja, hususan ya ardhini na baharini

Mohamed Abdirahman, afisa wa polisi katika mji wa Bula Hawo amesema waandamanaji hao wanaamini kuwa, raia watatu wa Somalia walitekwa nyara na askari wa kupambana na ugaidi wa Kenya siku ya Ijumaa na kisha kuuawa.

Duru zilizo karibu na Jeshi la Ulinzi ya Kenya (KDF) na Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) zimethibitisha habari ya kutokea makabliano hayo ya mtutu wa bunduki lakini hazijaeleza iwapo kuna askari waliouawa au kujeruhiwa.

Tags

Maoni