Oct 21, 2020 04:46 UTC
  • Wanamgambo wavamia jela DRC na kuachilia huru wafungwa 900

Wanamgambo waliokuwa na silaha wamevamia Gereza Kuu la Kangbayi katika mji wa Beni, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuachilia huru wafungwa 900.

Kwa mujibu wa taarifa, idadi kubwa ya wanamgambo walivamia gereza hilo, katika mji wa Beni mapema Jumanne na kuwaachilia huru wafungwa 900 kati ya 1,000 waliokuwa wanashikiliwa hapo.

Meya wa Beni Modeste Bakwanamaha amesema wanagamabo hao walivunja milango ya gereza kwa mashine za umeme. Aidha amesema wanaamini kuwa waliotekeleza hujuma hiyo ni wanamgambo wa kundi la ADF kutoka nchi jirani ya Uganda.

Waasi wa ADF nchini DRC

Kundi hilo limekuwa likiendesha shughuli zake mashariki mwa DRC tokea muongo wa 90. Hadi sasa hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na hujuma hiyo.

Idadi kubwa ya wangamabo walikuwa wanashikiliwa katika Gereza Kuu la Kangbayi, wakiwemo wafuasi wa ADF. Mwezi Juni mwaka 2017 wafungwa kadhaa walitoroka gereza hilo hilo baada ya hujuma ya wanamgambo wa ADF.

 

Tags

Maoni