Oct 25, 2020 07:52 UTC
  • Wananchi wa Morocco wapinga hatua yoyote ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni

Shakhsia wa kisiasa na kidini wa Morocco wamelaani hatua yoyote ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel. Wametoa tamko hilo katika mkutano wao kwa njia ya video.

Viongzi wa kisiasa na kidini wa Morocco wamelaani hatua za Rais Donald Trump wa Marekani za kuzishawishi baadhi ya tawala vibaraka za Kiarabu kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Shakhsia, taasisi na makundi mbalimbali ya kisiasa na kidini ya Mauritania, Algeria, Tunisia na Libya pia wameshiriki mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video. Taarifa ya mwisho ya mkutano huo imeeleza kuwa kisheria ni batili kuutambua rasmi utawala wa Kizayuni katika ardhi za Palestina na jambo hilo linakinzana na misingi mikuu ya kimaadili na haki za binadamu. 

Taarifa ya mkutano huo aidha umezitaka tawala za Kiarabu kutosalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani na kupinga suala la kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni. 

Wananchi na wanasiasa huru katika Ulimwengu wa Kiislamu wametoa radiamali yao hasi kwa njama za Marekani na Uzayuni ya kuanzisha uhusiano baina ya utawala wa Kizayuni na baadhi ya serikali vibaraka za Kiarabu. 

Wananch wa Morocco wakidhihirisha ghadhabu zao kwa kuchoma bendera ya utawala wa Kizayuni  

 

Tags