Nov 04, 2020 00:16 UTC
  • Rais Ouattara ashinda uchaguzi wa urais Ivory Coast, wapinzani walisusia

Rais Alassane Ouattara ameibuka mshindi katika uchaguzi wa rais nchini Ivory Coast huku wapinzani walioususia uchaguzi huo wakisema wataunda serikali ya mpito.

Tume Huru ya Uchaguzi (CEI) imetangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi, Oktoba 31 ambapo Ouattara ameibuka mshindi kwa 94.27% ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi. Henri Konan Bédié amepata asilimia 1.66, Kouadio Konan Bertin amepata asilimia 1.99 na Pascal Affi N’guessan amepata asilimia 0.99% ya kura zilizopigwa.

Tume hiyo imesema kiwango cha ushiriki kulingana na IEC ni 53.90%. Matokeo haya yanatarajiwa kuthibitishwa na Mahakama ya Katiba.

Waungaji mkono wa Alassane Ouattara 

Wapinzani Ivory Coast, ambao walisusia uchaguzi wa urais, wamesema wataunda serikali ya mpito.

Rais Ouattara, 78,  amekuwa madarakani kwa takriban muongo mzima, lakini anadai katiba mpya iliyoidhinishwa mwaka 2016 inamruhusu kugombea tena urais kwa muhula wa tatu.

Tags